Contact us: yuvinusm45@gmail.com | email: yuvinusm45@gmail.com

We're Coming Soon

Tutarudi Baada ya Matengenezo

Tupo kwenye matengenezo ya Mtandao Wetu Tutarudi Mchakato Ukishakamilika, Tunaomba Radhi kwa Usumbufu Utakaojitokeza!

We are working very hard on the new version of our site. It will bring a lot of new features. Stay tuned!


days

hours

minutes

seconds

Subscribe to our newsletter

Sign up now to our newsletter and you'll be one of the first to know when the site is ready:

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger
Design by Yuvinusm

5/7/16

Jason Rweikiza Achaguliwa Kuwa Katibu wa Wabunge wa CCMWABUNGE wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamemchagua Mbunge wa Bukoba Vijijini, Jason Rweikiza kuwa Katibu wao.

Rweikiza anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama, ambaye safari hii hakuwania nafasi hiyo.

Katika uchaguzi huo uliofanyika juzi usiku katika ukumbi wa Msekwa uliopo ndani ya viwanja vya Bunge, Katibu huyo mpya wa Wabunge wa CCM alikuwa akipambana na Mary Chatanda, Mariam Kisangi na Abdalah Ulega.

Wabunge wote wa CCM pia walipiga kura kuwachagua wabunge 10 kati ya 21 walioomba ujumbe wa NEC.

Waliochaguliwa ni Livingstone Lusinde, Dk Hamis Kigwangalla, Stanslaus Nyongo, Steven Ngonyani, Peter Serukamba, Faida Bakari, Agness Marwa, Munde Tambwe, Angella Kairuki na Jamal Kassim Ali.

Wabunge ambao kura hazikutosha ni Mbaraka Dau, Alex Gashaza, Hawa Ghasia, Ibrahim Raza, Profesa Norman Sigalla ‘King’, Almas Maige, Angelina Malembeka, Yahya Massare, Mattar Ali Salum na Hafidh Ali Tahir.