Contact us: yuvinusm45@gmail.com | email: yuvinusm45@gmail.com

We're Coming Soon

Tutarudi Baada ya Matengenezo

Tupo kwenye matengenezo ya Mtandao Wetu Tutarudi Mchakato Ukishakamilika, Tunaomba Radhi kwa Usumbufu Utakaojitokeza!

We are working very hard on the new version of our site. It will bring a lot of new features. Stay tuned!


days

hours

minutes

seconds

Subscribe to our newsletter

Sign up now to our newsletter and you'll be one of the first to know when the site is ready:

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger
Design by Yuvinusm

5/16/16

Je Ni Marafiki Wa Kweli? Njia 8 Za Kugundua Marafiki Bandia (Wanafiki)

Kila mtu ameshawahi kuwa na rafiki bandia kwa namna moja au nyingine. Rafiki bandia (fake), si rafiki, ni aina ya mtu ambaye huhitaji kitu kutoka kwako, kama vile umaarufu, pesa, n.k. Mara nyingi ni ngumu kutofautisha rafiki wa kweli na yule bandia. Makala hii inaelezea ni vipi utamgundua rafiki bandia, na kumkwepa mapema.
f3
Urafiki huja kwa kukutana na mtu na kujikuta wote mnapendelea vitu vya aina moja (Mfano, mpira, kusoma vitabu n.k.), hivyo mnajikuta mnajitofautisha na wengine na kuanzisha urafiki. Kitu ambacho huwa tunasahau ni kwamba, urafiki ni kupokea na kutoa. Unafanya kitu, na rafiki anafanya kingine, si kama jukumu, bali maelewano baina yenu yanapelekea hivyo. Ni hali Fulani ya kupeana support pindi kila mmoja anapohitaji.
Je nini kitatokea pale ambapo support na toa na pokea inaondoka, na inabaki pokea pokea tu? Ukiona hivyo ujue, urafiki huo umekwisha na si sahihi. Hivyo basi ujue unarafiki bandia. Vitu vifuatavyo vitakufanya ugundue, rafiki ulionao ni bandia:
  1. Mara kwa mara wanaahidi vitu hawavitekelezi: Mara kwa mara marafiki bandia hutoa sababu za kutofanya kile walicho ahidi. Hutoa sababu za kuahirisha jambo alilo kuahidi na kufanya uwe na shauku, na kibaya zaidi hushindwa kuhudhuria pale alipo ahidi kutokea, na hutoa ahadi nyingine kwamba ikitokea tena hatokuangusha.
  2. Muda wote, hutegemea wewe kuacha kilakitu na kuwatimizia mahitaji yao: Mara kadhaa hukupa ujumbe wa wewe kuwatimizia shida zao bila kujali kama unao muda wa kufanya hivyo. Na mara kwa mara unawasaidia, lakini kunakipindi huwezi wasaidia, kwa sababu ya kutingwa na mambo mengine ya kimaisha. Lakini wao hawajali kama unajambo jingine la kufanya na kuona jambo lao ni muhimu zaidi. Marafiki wapo kusaidiana, lakini si kwamba ndio itakuwa hivyo kila mara. Kushindwa kutambua hilo ni dalili ya kuwa rafiki huyo si sahihi.
  3. Wanapiga domo (umbea) muda wote kuhusu watu wengine: Hii ni dalili muhimu sana ya kumgundua rafiki bandia. Kama anaongelea sana kuhusu watu wengine, pata picha nini anasema juu yako kwao. Mara nyingi hufanya hivyo kutaka kujionyesha kwamba wao wapo juu zaidi kuliko wengine.
  4. Hutumia wema wako kama njia ya kutatua matatizo yao: Kwa kifupi ni kwamba, wanaona wema wako na wanatumia kujinufaisha. Huu ni ukweli usio pingika, rafiki bandia hukutumia vyovyote vile wanavyoweza kufanikisha mambo yao. Kama unafanya vizuri darasani, hujiweka karibu na wao waweze kufanikiwa. Ukiwalipia chakula au kitu kingine, wao huona ni sawa kwa sababu unao uwezo wa kufanya hivyo.
  5. Hawajali matizo yako: Mara nyingi, hii unaweza kuigundua kwa kupitia majibu wanayokupa pale unapowaeleza juu ya matatizo yako kwa njia ya text. Kwa mfano unapo tuma text na wao kujibu tu, “oh”, “damn”, au “k”. Marafiki wanamna hii si wazuri, kwani rafiki wa kweli huchukua tatizo lako kwa uzito stahiki.
  6. Hukutafuta pale tu wanapohitaji kitu kutoka kwako: Hata kama wewe ndio mtu pekee unayeweza kumsaidia kupata au kutatua tatizo alilonalo, si vyema kukutafuta kila mara anapokuwa na shida. Rafiki wa kweli si mara zote hukutafuta kwa shida, mara nyingine hukutafuta kwa kukujulia hali. Mfano anaweza kukutumia text kukushukuru tu, “mambo vp jay, shukrani kwa usafiri jana, uko poa lakini?”. Si kitu kibaya kumsaidia rafiki, lakini kama rafiki huyo, mara kwa mara anakuwa akikutafuta kwa ajili ya shida zake kuliko urafiki, ujue huyo si rafiki wa kweli.
  7. Huonyeshwa kutokupendezwa na mazuri ufanyayo au upatayo: Unapo washirikisha taarifa nzuri ya mafanikio, au ya furaha kwako, wao hutafuta jinsi ya kuifanya taarifa hiyo ni ya kwaida na wao wamefanya zaidi ya hivyo. Mfano; “ndugu nimepata kazi, sawa mimi nimepandishwa cheo” au “Nimenunua gari, ok mmi nimenunua gari na nyumba”. Siku zote hutafuta kitu cha zaidi yako, kwa sababu hawaoni taarifa yako nzuri ni kitu cha kufurahia.
  8. Hukusifia na kukung’ong’a wakati mmoja: Hiki ni kitu kibaya sana kutoka kwa Yule uliyedhani ni rafiki wa kweli, hujifanya kutabasamu na kukusupport kwa kila unachofanya ili hali wanachukizwa moyoni. Mara kadhaa huongea maneno ya kukufanya ujisikie vibaya. Mfano wa maneno ya maudhi; “Hiki chakula kitamu, nani amekupikia?”, au “Text yako nzuri sana, umeicopy wapi?”. Hutafuta njia ya kukung’ong’a katika vitu vizuri kwako.