5/9/16

Jinsi Mwadui Ilivyoihakikishia Ubingwa Yanga

 

Najua unajua kama Ligi zote duniani zinaelekea mwisho na tayari Ligi kama EPL, Bundesliga,Serie A na Ligue 1 zimeshapata wababe. Sasa achana nazo hizo za Ughaibuni njoo Bongo tuipongeze Yanga kwa kutwaa ubingwa. Ligi bora Afrika Mashariki na kati nayo tayari ishatoa bingwa tena zikisalia mechi 3 huku bingwa wa kihistoria Dar Young Africans akitetea taji lake mara  ya pili mfululizo.

NAMNA WALIVYOCHUKUA KAMA LEICESTER CITY

Yanga ilihitaji alama tatu tu ili itangaze ubingwa lakini Mwadui Fc imefanya yaliyofanywa na Chelsea kwani ubingwa wa Yanga umenogeshwa na Mwadui FC baada ya kuilaza Simba bao 1 – 0 kwenye Uwaja wa Taifa na kuifanya Yanga ifikirie mchezo wake wa Marudio dhidi ya Sagrado Esparanca na si ligi tena.

YANGA INAELEKEA WAPI?

Hakuna fitina Yanga ilikuwa vizuri msimu huu kuanzia nje ya uwanja hadi ndani anayeingia na anayetoka wote ni wakali. Siku zote timu bora ndiyo inayopata mafanikio, Yanga itakwea pipa mwakani kuwakilisha nchi Ligi  ya Mabingwa Barani Afrika ikiwaacha watani wake wakiwa hawana nasafi ya kuwakilisha nchi kwa mara ya tatu mfululizo. Azam imeharibu  mechi za nwishoni na kocha wao amesema wazi baada ya fainali ataachana na timu hiyo.

MECHI ZILIZOBAKI NA KANUNI

Yanga anaenda kucheza na Mbeya City  Mei 14 lakini ataweza kuchezesha timu  B ili  timu yake ipumzike kwa ajili ya michuano ya kimataifa. Kwa kawaida mechi zote zilizobaki Yanga inatakiwa wapigiwe makofi na timu atakazocheza nazo kuonesha kukubali alichokifanya Yanga msimu huu.

Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts