5/1/16

JPM: Askari Aliyetukanwa na Mke wa Waziri Apandishwe Cheo

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amemuagiza Kamishna wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernesti Mangu kumpandisha cheo mara moja askari wa Usalama Barabarani ambaye alitukanwa na Mke wa Waziri wakati akitekeleza majukumu yake ya kazi.

Rais ameyasema hayo wakati akifungua Kikao cha Makamanda wa Polisi wa Mikoa na kusema tayari amekwishamuonya Waziri huyo ambaye mke wake alimtusi Askari wa Usalama Barabarani.

Wakati akitoa agizo hilo, Rais Magufuli amesema hakuna kiongozi au familia ya kiongozi iliyo juu ya sheria.

Chanzo: TBC1

Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts