5/17/16

KAFULILA ashindwa kesi ya ubunge
Mbunge Kigoma Kusini Hasna Mwilima kupitia tiketi ya CCM ameshinda kesi ya uchaguzi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa jimbo hilo, David Kafulila (NCCR-Mageuzi).

Mahakama Kuu Kanda ya Tabora imesema Kafulila na mashahidi wake wameshindwa kuthibitisha madai kwamba alimshinda mpinzani wake, hivyo Mwilima ndiye mshindi halali.
Hata hivyo, Kafulila amesema hakubaliani na hukumu hiyo na kuahidi kukata rufaa, jambo linaloungwa mkono na wafuasi wa chama chake na Ukawa kwa ujumla.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts