5/24/16

Karani Imtu Afungwa Jela Miaka 27
Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemhukumu Karani wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia (Imtu), Bakari Mlanga (23) kifungo cha miaka 27 jela baada ya kupatikana na hatia ya kughushi fomu za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).


Pia, Mahakama hiyo imemhukumu mkazi wa Manzese, Ahmed Mbinjika (25) kifungo cha miaka 12 baada ya kupatikana na hatia hiyo.


Katika kesi hiyo, mshtakiwa wa kwanza alikuwa anakabiliwa na mashtaka tisa na kila shtaka atatumikia kifungo cha miaka mitatu, huku mshtakiwa wa pili alikuwa anakabiliwa na mashtaka manne na kila moja atatumikia kifungo cha miaka mitatu na kwamba, adhabu hizo zinakwenda pamoja.


Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Juma Hassan alisema upande wa mashtaka ulileta mashahidi watano kuthibitisha mashtaka hayo na Mahakama imeridhika na ushahidi.


Alisema upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha mashitaka yao bila ya kuacha shaka hivyo.


Awali, Wakili wa Serikali, Florida Wenslaus alidai Desemba 15, 2014 washtakiwa walighushi fomu ya NHIF ya Tito Mfilinge ili kuonyesha kuwa imesainiwa na Dk Emma Chambenga na ni halali kutumika.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts