5/29/16

Kessy : Niko 'fiti' kuitumikia Yanga


BEKI mpya wa klabu ya Yanga, Hassan Kessy amesema kuwa yupo tayari kuanza kuitumikia timu yake hiyo kutokana na kufanya mazoezi kwa muda mrefu.
BEKI mpya wa klabu ya Yanga, Hassan Kessy
Kauli hiyo ya Kessy ni kama 'dongo' kwa klabu yake ya zamani ya Simba ambayo ilimuacha kwa kumpa adhabu kutoka na kile kinachoelezwa kuwa ni utovu wa nidhamu.
Akizungumza na gazeti hili jana, Kessy alisema kuwa alikuwa akifanya mazoezi kwa muda mrefu ili kulinda kiwango chake kwa ajili ya kumvutia kocha wake mpya Mdachi Hans van der Pluijm.
"Mimi ni mchezaji na kazi yangu ni hii, hata kocha wangu akiniambia leo (jana) niingie uwanjani nipo tayari na bado nitapiga mzigo wa maana," alisema Kessy.
Beki huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar aliwapongeza wachezaji wenzake wa Yanga kwa kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho (FA) baada ya kuifunga Azam magoli 3-1 Jumatano iliyopita huku pia wakitetea ubingwa wa Bara.
Beki huyo ambaye bado hajapata namba ya kudumu katika timu ya Taifa (Taifa Stars) alisaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Yanga
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts