5/25/16

Kufungwa na Yanga Mara Mbili Ilikuwa Soo Kwetu-Mgosi

 

Musa Hassan Mgosi amesema kuwa kitendo cha kufungwa mara mbili na watani wao wa jadi kwenye mechi ya Simba na Yanga kilimuumiza sana na anaamini kuwa kitendo hicho kitawatokea Yanga kwa namna nyingine.

“Vipo vitu vingi sana vimenikwanza kwenye msimu huu lakini vikubwa sana ambavyo siwezi kuvisahau ni mechi ya Coastal Union ilikuwa mechi ya nusu fainali, timu kama ile ilikuwa si timu ya kututoa kwenye mashindano lakini ilifanya vile kutokana na mchezo kwani mchezo hauna timu kubwa wala ndogo ni kutokana na vile ulivyojianda,” alisema Mgosi.

Mbali na hilo Mgosi alionyesha wazi kuwa Simba kufungwa mfululizo na Yanga kwake ni maumivu makali na jambo ambalo bado linamsumbua mpaka sasa na kuamini kuwa machozi aliyoyatoa yatakuja kujirudia kwao Yanga.

“Kitu ambacho kiliniumiza sana ni mechi kati ya Simba na Yanga maana ni timu ambazo zina mashabiki wengi Tanzania, katika uwepo wangu wote Simba haijawahi kutokea Simba kufungwa mara mbili mfululizo na Yanga, hivyo kitendo hicho kiliniumiza sana naamini chozi langu lile litarudi tena kwao wao kwa namna nyingine mpaka leo nitaendelea kuumia sababu haijawahi kutokea kipindi chote nipo na Simba,” alisisitiza Mgosi.

Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts