5/24/16

LOWASSA- Asanteni kwa Kunifuata

 

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa amewataka Watanzania kuwa na imani na Chadema kwa kuwa maeneo yanayoongozwa na chama hicho katika halmashauri na majimbo yana maendeleo tofauti na maeneo mengine.

Lowassa ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Moita Bwawani ambapo pamoja na mambo mengine amewashukuru wananchi waliompigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.”Wanakuja Simanjiro, Kiteto, Ngorongoro, Longido hawatuwezi na wakitaka waje maeneo haya walinganishe na maeneo yao hawatuwezi, ninawashukuru sana kwa kuhama na mimi toka CCM kwenda Chadema”- Amesema Lowassa.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Salum Mwalimu amesema chama chao siyo chama cha upembuzi yakinifu na urasimu bali chama chao ni chama cha kufanya kazi kwa vitendo ambapo watahakikisha wanapeleka maji eneo la Moita Bwawani.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli Isack Joseph amewataka watendaji na wenyeviti wa vijiji kutoruhusu wakandarasi kufanya kazi bila wao kupata barua na kujiridhisha na miradi itakayotekelezwa na kuhakikisha wanaisimamia ili iwe na tija kwa wananchi.

Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts