MABINGWA LECEISTER CITY WAZINDUA JEZI ZAO MPYA BILA KUWEPO RIYAD MAHREZ | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

5/6/16

MABINGWA LECEISTER CITY WAZINDUA JEZI ZAO MPYA BILA KUWEPO RIYAD MAHREZ


Leceister,England.

Mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya England Leceister City leo wamezidua jezi zao mpya watakazozitumia katika msimu mpya wa 2016-17 katika michuano ya Ligi Kuu na ile ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Katika uzinduzi huo uliofanyika katika makao makuu ya klabu hiyo King Power nyota wake Ryad Mahrez hakuwa sehemu ya wachezaji waliotumika kutambulisha jezi hizo hali iliyozua hofu kuwa mchezaji huyo toka Algeria ana mpango wa kuihama klabu hiyo.

Wachezaji waliotumika kutambulisha jezi hizo zilizotengeneza na kampuni ya PUMA ni mlinda mlango Kasper Schmeichel,nahodha na mlinzi Wes Morgan pamoja na washambuliaji Shinji Okazaki na Jamie Vardy.google+

linkedin