5/12/16

MADEE KUACHIA NGOMA ALIYOFANYA NA MSANII WA NIGERIA

 

Hamadi Ali a.k.a Madee jina ambalo sio geni   masikioni mwa mashabiki wa muziki wa Bongo Flava, alichafua hali ya hewa kipindi alipoamua kuachana na ngumu nyeusi hapa nazungumzia muziki wa Hip Hop na kurejea kwenye Bongo Fleva huku akitoa nyimbo ya Hip Hop haiuzi na kuibua tafarani kubwa.

‘Collabo’ ni moja ya vitu vinavyoweza kumsaidia msanii kuzidi kufahamika zaidi kitaifa na kimataifa ingawa inaweza ‘kuhit’ ama ‘isihit’. Hivi karibuni Madee aliwahi kufanya vizuri katika game baada ya kufanya Collabo ya kwanza na wasanii wa nchini Kenya P- Unit katika remix ya nani kamwaga pombe yangu.

Madee amejipanga upya baada ya kimya cha muda mrefu kwa kutoa nyimbo ya Migulu Pande ili awatulize mashabiki zake wakati akiendelea na mipango mingine; tayari Madee amesema kuwa ngoma atakayoiachia hivi karibuni inayokwenda kwa jina la Aisha amefanya na msanii kutoka Nigeria Tecno na kinachosubiriwa ni video ya ngoma hiyo iliyotengenezwa na Tecno huku vocal ikiingizwa na Tuddi Thomas.

“Ngoma yangu inayofuata nimefanya na Tecno inaitwa Aisha inahusu mapenzi ngoma iko tayari kilichobaki video, beat ya ngoma hiyo ameifanya Tecno … ni ngoma ya Madee”  alisema Madee

Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts