5/3/16

Mama wa Tupac Afariki dunia


Mama wa msanii Tupac ambaye pia ni mwanaharakati Afeni Shakur Davis amefariki dunia katika jiji la Calfonia Nchini Marekani.
Afeni Shakur amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 69.
Kwa mujibu wa taarifa za awali ni kwamba mama huyo alifikishwa hospitalini saa 9:34 usiku na aliaga dunia majira ya saa 10.38 usiku wa jumatatu.
Chanzo cha kifo chake bado hakijajulikana ambapo madaktari wanaendelea na uchunguzi kubaini kiini cha kifo hicho.
Shakur Davis alikuwa ni ngao ya marehemu mwanae ambapo Tupac aliimba wimbo maarufu alioupa jina la 'Dear Mama' ambapo baada ya kifo cha Tupac mwaka 1996 mama huyo kwa kutumia mali alizoacha mwanae na kunda taasisi inayoitwa Tupac Amaru Shakur Foundation inayosaidia kuinua vipaji vya watoto.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm