Nafasi ya Manchester United kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya UEFA kwa msimu ujao imemalizika katika mchezo wa Bournemouth baada ya kuibuka na ushindi wa goli 3-1 na ikiwa inahitaji kupata magooli 19 ili kuipita Manchester City ambayo walikuwa na alama sawa wakiwa na tofauti ya magoli.
Magoli ya Man United katika mchezo huo wa Bournemouth yalifungwa na Wayne Rooney, Marcus Rashford na Ashley Young na goli pekee la Bournemouth akijifunga beki wa Man United, Chris Smalling baada ya kupigwa mpira ambao ulimgonga na kuingia golini.
Baada ya matokeo hayo, sasa Manchester United itashiriki Ligi ya Vilabu Barani Ulaya (UEFA Europa League) kwa msimu ujao baada ya kukosa alama ambazo zingewawezesha kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.