5/9/16

Matukio Makubwa Yaliotokea Duniani Siku Kama ya Leo

 dunia

Mei 9 mwaka 1950 Azimio la Schumann

Mei 9 mwaka 1950 Azimio la Schumann  ambalo pia linatambulika kama Azimio la Mei 9 ni azimio ambalo ni kitovu cha kuundwa kwa Ulaya.

Azimio hilo lilitambulishwa na Robert Schumann ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa.

Waziri huyo alilitambulisha azimio hilo katika Jumba la Mikutano la Quai d’Orsay, mjini Paris.

Azimio hilo lilitoa fikra kwa Jean Monnet na kupendekeza  uundwaji wa  Shirikisho la Ulaya litakalo weka pamoja mapato yanayotokana na makaa ya mawe Ujerumani na Ufaransa na kutiwa saini Aprili 18 mwaka 1951 na kuunda shirikisho la makaa ya mawe na chuma Ulaya.

Shirikisho hilo lilijumuisha nchi 6 za Ulaya.

Mei 9 mwaka 1942  Vedat Tek alifariki dunia

Mei 9 mwaka 1942 Mhandisi mashuhuri kutoka Uturuki kwa jina la Vedat Tek alifariki dunia mjini Istanbul.

Vedat Tek ni miongoni mwa wahandisi hodari nchini Uturuki  ambaye alifahamika kwa kazi zake za uhandisi na kuboresha  ufundi wake nchini Uturuki.

Baada ya kumaliza kisomo chake katika shule ya ufundi mwaka 1898 alirejea katika kazi yake mjini Istanbul.

Vedat Tek alifanya kazi kama mwalimu katika kitengo cha ujenzi  katika kipindi hicho.

Majengo mengi ya kifahari katika ardhi ya Uturuki pia baadhi yake yalijengwa na mhandisi huyo ambae ni mashuhuri katika historia ya ujenzi.

Baadhi ya kazi zilizosimamiwa na mhandisi huyo limo jengo la la bunge linalopatikana mjini Ankara katika tarafa ya Ulus, msikiti wa Pasha na Cemil Topuzlu.

Mei 9 mwaka 1945 Siku ya Ushindi

Mei 9 mwaka 1945 tarehe ambayo Vita vya Pili vya Dunia wanazi na Jeshi la Kisoviet walipambana na jeshi la kisoviet kupata ushindi.

Tarehe hiyo ilipewa jina la Siku ya Ushindi.

Nchi nyingi huadhimisha Siku ya Ushindi barani Ulaya.

Mei 9 mwaka 1978 Waziri Mkuu wa Italia Aldo Moro alifariki

Mei 9 mwaka 1978 Waziri Mkuu wa Italia Aldo Moro alikutwa amefariki baada ya mwili wake kukutwa katika gari mjini Roma nchini Italia.

Inasemekana kuwa waziri huyo alitekwa na wanaharakati wa kisiasa Machi 16 na kutafutwa kwa muda wa takriban miezi miwili.

Jeshi la Polisi nchini Italia lilifanya uchunguzi bila ya mafaanikio na baadae kumpata akiwa amefariki.

Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts