Matukio ya Picha Bungeni Leo Mjini Dodoma. | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

5/16/16

Matukio ya Picha Bungeni Leo Mjini Dodoma.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Katiba, Mhe. Najma Giga wakielekea Bungeni kwa ajili ya vikao vya asubuhi vya Bunge hilo leo 16 Mei, 2016 mjini Dodoma.  

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako (kulia) pamoja na Naibu Waziri, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Edwin Amandus Ngonyani wakielekea Bungeni kwa ajili ya vikao vya asubuhi vya Bunge hilo leo 16 Mei, 2016 mjini Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kulia) pamoja na Mbunge wa Viti Maalul CCM, Mhe. Halima Bulembo wakielekea Bungeni kwa jili ya vikao vya asubuhi vya Bunge hilo leo 16 Mei, 2016 mjini Dodoma.

Baadhi ya Viongozi wa Jeshi la Polisi, Magereza, Uhamiaji na Zimamoto wakiingia ndani ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma kwa ajili ya vikao vya bunge hususan kusikiliza Bajeti ya Wizara ya Mambo y Ndani ya Nchi 16 Mei, 2016 mjini Dodoma.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mikoa (OR-TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo akijibu baadhi ya hoja za Wabunge Bungeni mjini Dodoma.

Baadhi ya Wanafunzi pamoja na wageni wengine waalikwa wakifuatilia vikao vya Bunge mjini Dodoma 16 Mei, 2016.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kushoto) pamoja na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mwigulu Nchemba wakiteta jambo Bungeni mjini Dodoma.

Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo akijibu baadhi ya hoja mbalimbali za Wabunge kuhusiana na Wizara yake leo bungeni mjini Dodoma.
(Picha zote na Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma)

google+

linkedin