5/12/16

Mchungaji Akamatwa na Meno ya Tembo

Jeshi la Polisi Mkoani Katavi linawashikilia watu wawili akiwemo Mchungaji wa Kanisa la Monrovian mkoani humo baada ya kukutwa na vipande kumi na moja vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 20.3.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda, amesema vipande hivyo vimekutwa ndani ya mfuko wa sandarusi na kuwekwa ndani ya kanisa hilo ambapo polisi walipata taarifa ya uwepo waa nyara hizo za serikali.

Kamanda Nyanda amesema watuhumiwa hao wote walikamatwa katika Kitongoji cha Tombola, Kijiji cha Usevia, Tarafa ya Mpimbwe na kwamba vipande hivyo vilikuwa vimehifadhiwa kwa lengo la kusafirisha.

Katika hatua nyingine jeshi hilo linamshikilia mtu mmoja kwa kukutwa na jino la Simba katika Kijiji cha Sitarike maeneo ya Ngoroka baada ya jeshi hilo kufanya operesheni maalum katika eneo hilo.

Aidha, katika msako mwingine Kamanda Nyanda amesema wanamshikilia mtu mmoja kwa kukutwa na risasi pamoja na bunduki ya SMG, akiwa ameihifadhi ndani kwake.

Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm