5/3/16

Mkutano mkuu wavurugika Geita

Mkutano Mkuu wa kupiga kura ya kutokuwa na imani na mwenyekiti wa kijiji cha Nyakamwaga wilayani Geita, Abdul Kalakiza umevurugika baada ya wananchi kung’ang’ania kupiga kura bila utaratibu wa kisheria, hali ambayo imesabaisha zoezi hilo liahirishwe.

Vurugu zilizosababisha mkutano huo kuvunjika zimetokea jana jioni mbele ya Mkuu wa wilaya ya Geita, Omary Mangochie, aliyehudhuria Mkutano huo kwa lengo la kumaliza mgogoro huo uliodumu kwa kipindi cha miaka mitatu.

Mara baada ya vurugu hizo, Mkuu huyo wa Wilaya alilazimika kuahirisha zoezi la uchaguzi huo.

Wananchi walikuwa kwenye mkutano huo wamesema uwamuzi uliochukuliwa na mkuu wa wilaya hiyo wa kuahirisha uchaguzi huo kwani ungeleta vurugu kubwa kijijini hapo.

CHANZO: CHANNEL TEN
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts