5/16/16

Mkuu wa Upelelezi wa Dar Aondolewa Kosa la Mauaji.

 

Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) amemuondolea kosa la mauaji aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Zombe na sasa inataka ajibu mashtaka ya kuficha wahalifu.

DPP ameitaka Mahakama imtie hatiani kwa kosa la kuwalinda wahalifu ambao walitenda kosa la mauaji ya wafanyabiashara na dereva wa teksi.

DPP amefanya mabadiliko hayo kwenye rufaa aliyoikata Mahakama ya Rufani dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu wa kumuachia huru Zombe, ambaye alikuwa Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) katika mashtaka ya mauaji.

Awali, DPP alikata rufaa akipinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyomwachia huru Zombe na wenzake tisa, katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge Mkoani Morogoro na dereva mmoja wa teksi wa Manzese Jijini Dar es Salaam.

Katika rufaa hiyo, DPP  aliiomba Mahakama ya Rufani iwatie hatiani washtakiwa hao kwa kosa la mauaji ya kukusudia, kama ilivyokuwa kwenye kesi ya msingi, kosa ambalo adhabu zake ni pamoja na kunyongwa hadi kufa.

Credit:JF
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts