Contact us: yuvinusm45@gmail.com | email: yuvinusm45@gmail.com

We're Coming Soon

Tutarudi Baada ya Matengenezo

Tupo kwenye matengenezo ya Mtandao Wetu Tutarudi Mchakato Ukishakamilika, Tunaomba Radhi kwa Usumbufu Utakaojitokeza!

We are working very hard on the new version of our site. It will bring a lot of new features. Stay tuned!


days

hours

minutes

seconds

Subscribe to our newsletter

Sign up now to our newsletter and you'll be one of the first to know when the site is ready:

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger
Design by Yuvinusm

5/27/16

Mramba ashauri Tanesco isimiliki mitambo IPTL


MKURUGENZI Mtendaji wa shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Injinia Felchesmi Mramba amesema kama akiulizwa serikali inunue ama isinunue mitambo ya kuzalisha umeme ya Independet Power Tanzania Limited (IPTL), angeshauri ibaki kwa mwekezaji husika kwa sababu ni gharama kubwa zaidi kuiendesha.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalum na wahariri wa magazeti ya Kampuni ya The Guardian ofisini kwake, Mramba alisema kununua mitambo ya IPTL hakutaendana na thamani ya fedha.
Katika moja ya maamuzi yake kuhusu sakata la Fedha za Tegeta Escrow zilizochukuliwa kutoka Benki Kuu, Bunge mwaka jana lilipitisha azimio la serikali kuitaifisha mitambo ya IPTL.
Aidha, wanasiasa kadhaa wamekuwa wakipendekeza serikali inunue mitambo hiyo kutoka kwa mwekezaji ili kukwepa tozo ya uwekezaji (capacity charge) ambayo hulipwa nje ya bei ya manunuzi ya umeme.
"Ukinununa mitambo ya Iptl utakuwa unanunua mashine za zamani... lini imeanza kutumika? Mwaka 1998. Hivyo hutapata 'value for money' (hakutaendana na thamani ya fedha)," alisema Mramba.
Aidha, Mramba alisema kununua mitambo hiyo sasa hakutakuwa na faida kwa nchi kwa sababu inatumia mafuta kuchakata umeme.
Njia nzuri ya kupata matumizi bora ya mtambo wa IPTL, alisema Mramba ni kuhakikisha unabadilishwa na kuwa wa kutumia gesi kuzalisha umeme ambapo itauza unit mja kwa senti ya Marekani 8-9 badala ya senti 19-20 za sasa.
Alisema mbali na gharama za uendeshaji mitambo ya mafuta, pia serikali italazimika kugharimia matengenezo ya mara kwa mara na ununuzi wa vipuri pindi mitambo hiyo itakapoharibika.
Aidha, Mramba alisema baada ya kubaini mikataba mingi iliyoingiwa ikiwemo wa IPTL na kampuni ya kufua umeme kwa njia ya gesi asilia, Songas Limited, inamapungufu makubwa, wameanza kuwaita wahusika ili kuangalia uwezekano wa kuirekebisha.
Moja ya udhaifu waliobaini ni kuwa mikataba hiyo haitoi mwanya wa wabia kujitoa endapo hawajaridhishwa na ufanisi.
Pia, miaktaba hiyo, haielezi nini cha kufanya baada ya mikataba kuisha kama je serikali ichukue mitambo au makampuni hayo yataendelea kuiuzia umeme Tanesco bila tozo ya capacity charge.
“Bahati nzuri mikataba miwili imeisha ambayo ni ya (wawekezaji wa dharura) Symbion na Aggreko," alisema.
"Lakini hii miwili ya IPTL na Songas tumewaita wahusika ili tukae pamoja kuwaeleza mapungufu tuliyoyabaini na kutafuta njia ya kurekebisha kwa pamoja.
“Mikataba tunayoingia ipo ya aina mbili, ile ya wawekezaji binafsi ya umeme ambayo muda wake huchukua miaka 20; kama wa IPTL tuliingia mwaka 2002 na itaisha 2022 na Songas tuliingia 2004 itaisha 2024, na mkataba wa pili ni wa dharura kama ile ya Symbion na Aggreko iliyoisha.”
WADAIWA
Alisema kwa upande Tanzania bara serikali imeshalipa Sh. Bilioni 163 na deni lililobaki sio la malimbikizo kama hapo awali.
“Zanzibar tunaidai zaidi ya Sh. bilioni 80 lakini vipo vikao tunavyokutana mara kwa mara wao ili waweze kulilipa deni hilo,” alisema.
LUKU
Mramba alisema mpaka sasa wameunganisha mita za luku kwa asilimia 90 na wanatarajia mwishoni mwa mwaka huu watamalizia asilimia zilizobaki.