5/1/16

Mzee Majuto Atangaza Kustaafu Kuigiza

Siku ya kwanza ya May 2016 jina la Mzee Majuto limetajwa tena kwenye vichwa vya habari kuhusu kuacha kwake kuigiza, kama utakumbuka aliwahi kuongea na Millard Ayo mwaka 2014 na kusema angestaafu kuigiza mwaka 2015 lakini hakustaafu, akaendelea na movie zake.
Kauli yake mpya leo May 1 2016 kupitia Instagram ya CloudsFM kuna maelezo yafuatayo >>> ‘Gwiji la sanaa ya maigizo nchini Amri Athmani aka Mzee Majuto ametangaza rasmi kustaafu kuigiza na kutumia muda wake kumtumikia mola wake. Majuto amekuwa akifanya sanaa hii ya maigizo kwa muda mrefu na alianza kupata umaarufu mwanzoni mwa miaka ya 90’
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm