5/16/16

Nay Wa Mitego: Ngoma ya Salaam Zao iliniweka kwenye wakati mgumu sana kuliko nyimbo zangu zote
Mkali wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego amefunngua kuwa ingawa asilimia kubwa ya ngoma zake zinazofanya vizuri ni zile ambazo inaonekana amediss watu live kwa kuwataja majina lakini katika maisha yake anasema hatoisahau wimbo wa Salaam Zao kwa sababu ndiyo wimbo iliyowahi kumpa shida kuliko nyimbo zake zote.

‘’Ngoma ya Salam Zao nilipokea vitisho vingi sana,kwasababu kwanza nakumbuka kuna mmoja kati ya watu niliowataja alishawalipa mawakili na mmoja kati ya hao mawakili alikuwa ni shabiki wangu akaniambia mpaka muda huo kuna mawakili kama watatu wameshalipwa hela natakiwa kwenda mahakamani akaniambia nijipange kama nina wakili nijiandae kwenda mahakamani’’ Alisema Nay Wa Mitego.

‘’Yule wakili alinihakikishia kwa kitu ambacho nimeimba wao walikuwa wakifanya vile kwasababu wamelipwa nikiwa na wakili mzuri nilikuwa sina kesi,iliniletea shida sana lakini kwasababu huwa najua ni kitu gani nafanya na kabla sijaimba huwa nafanya uchunguzi kwahiyo huwa najipanga kabisa litakalonitokea baada ya ngoma kutoka’’ Aliongeza Nay Wa Mitego.

Source: Cloudsfm
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts