5/18/16

Nick wa Pili akanusha kumwandikia Joh Makini mashairi

Joh Makini aliongelea issue kuwa kuna watu wanadhani yeye huandikiwa mashairi na mdogo wake Nick wa Pili kwenye ngoma yake Don’t Bother.
13116835_817495615050905_1981597518_n
Na sasa Nick amezungumzia jambo hilo analolielezea kama ni propaganda. Amesema Joh alianza kuhit na nyimbo kibao kama Chochote Popote na album ya Zamu Yangu kipindi ambacho hakuna alikuwa akimfahamu yeye na alikuwa hawezi kuandika kama kaka yake.
“Sijui ni nani alianzisha hiyo propaganda, ni kama hiyo propaganda ya kuwa Weusi wanabebwa. Ni rahisi sana kusema Weusi wanabebwa, ni ngumu sana kusema Don’t Bother wanabebwa, ngumu kusema Baba Swalehe anabebwa lakini unaposema Weusi unakuwa unabebwa ukweli,” Nick aliiambia 255 ya XXL kupitia Clouds FM.
“Joh Makini anajiandikia mwenyewe lakini sisi kama Weusi tukiwa studio tunasaidiana mashairi hilo liko wazi, nilishasaidiwa sana, kila mtu alishawahi kusaidiwa sana, hauwezi kuwa unajua kila kitu,” amesisitiza Nick.


Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts