5/4/16

Ningekuwa CCM ningehoji kutorushwa Bunge 'live'


Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Fredrick Sumaye amesema kwamba hata kama angekuwa katika chama cha mapinduzi (CCM) angehoji kutorushwa kwa Bunge live kwani ni haki ya kikatiba.
Sumaye ameyasema hayo alipokuwa akiadhimisha uhuru wa vyombo vya habari jijini Dar es salaam ambapo amesisitiza kuwa kupata habari ni haki ya wananchi ya kikatiba hivyo kukataza Bunge ni kuwanyima wananchi haki yao ya msingi.
''Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasisitiza kulinda uhuru wa vyombo vya habari, na kuwaenzi wanahabari ambao huhatarisha maisha yao hivyo hata kama ningekuwa CCM lazima ningehoji kutorushwa kwa Bunge live''- Amesema Sumaye.
Ikumbukwe kuwa Sumaye kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 alitangaza kuunga mkono mabadiliko na kujiondoa katika chama chake cha awali CCM ambapo hadi sasa bado hajatangaza chama ambacho atajiunga nacho au kurejea CCM.
 -EATV
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm