Contact us: yuvinusm45@gmail.com | email: yuvinusm45@gmail.com

We're Coming Soon

Tutarudi Baada ya Matengenezo

Tupo kwenye matengenezo ya Mtandao Wetu Tutarudi Mchakato Ukishakamilika, Tunaomba Radhi kwa Usumbufu Utakaojitokeza!

We are working very hard on the new version of our site. It will bring a lot of new features. Stay tuned!


days

hours

minutes

seconds

Subscribe to our newsletter

Sign up now to our newsletter and you'll be one of the first to know when the site is ready:

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger
Design by Yuvinusm

5/27/16

Polisi yaahirisha kumhoji Maalim Seif

 

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad
Jeshi la Polisi Zanzibar limeahirisha kumhoji Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad kwa sababu zilizoelezwa kuwa nje ya uwezo wake.
Katika barua yake kwa Maalim Seif iliyosainiwa na DCP Salum Msangi kwa niaba ya Kamishna wa Polisi Zanzibar, haikutaja ni lini mahojiano hayo yatafanyika lakini imesema, “Tutakujulisha mapema siku ya mahojiano itakayofuata mara baada ya kukamilisha taratibu”.
Barua hiyo ya Mei 26 imenukuu barua ya awali ya Mei 22, 2016 iliyomuita mwanasiasa  huyo makao makuu ya polisi Zanzibar kwa mahojiano kuhusu, “masuala mbalimbali yanayohusu ulinzi na usalama wa visiwa hivi.”
Kutokana na hatua hiyo, Maalim Seif aliyetarajiwa kuwasili saa 3 asubuhi Zanzibar kutoka Dar es Salaam kwa ajili ya kuhojiwa aliahirisha safari hiyo na atawasili Saa 10 za jioni kwa ajili ya maandalizi ya ziara yake ya kichama kuanzia kesho katika wilaya  saba za Unguja.