5/15/16

Rais wa Zamani wa Argentina Huenda Akafungwa Gerezani Kwa Miaka 20

 

Rais wa zamani wa Argentina Cristina Fernandez de Kirchner, ameshtakiwa kwa tuhuma za ufisadi katika awamu yake ya uongozi nchini.

Kirchner anadaiwa kudhibiti soko la ubadilishanaji wa fedha za kigeni nchini Argentina kinyume cha sheria wakati alipokuwa madarakani.

Mashtaka zaidi yamebainisha kwamba Kirchner alihusika katika mikataba ya mikopo ya fedha dola bilioni 15 kutoka benki kuu ya nchi aliyoitoa kwa watu wasiojulikana kwa thamani ndogo ya dola.

Hali hiyo ya uuzaji wa fedha kwa thamani ya chini zaidi ya wastani ilisababisha sarafu ya nchi kushuka kwa kiasi kikubwa.

Kwa mujibu wa taarifa za BBC, kiongozi huyo pia alihusika na utapeli wa fedha dola bilioni 5.2 dhidi ya viongozi 12 wa serikali akiwemo waziri wa zamani wa uchumi Axel Kicillofna mkurugenzi wa benki kuu Alejandro Vanoli.

Licha ya mashtaka hayo, Kirchner amekanusha kuhusika na ufisadi na kujitetea kwamba anafanyiwa dhulma za kisiasa.

Kosa la utapeli nchini Argentina hutolewa hukumu ya kifungo cha kati ya miaka 5-20 gerezani.

BBC

Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts