5/22/16

RUNGWE Atoa ya Moyoni Kuhusu Kutumbuliwa kwa KITWANGA.


Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) kimesema kinaunga mkono uamuzi wa Rais Dk. John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Charles Kitwanga kwani kiongozi wa umma kuingia bungeni akiwa amelewa si sahihi na haileti picha nzuri kwa wanachi wanaowategemea wao kama watunga sera wa nchi.
Mwenyekiti wa Chauma Hashim Rungwe ameitoa kauli hiyo na kuongeza kuwa baadhi ya viongozi wanawakatisha tamaa wananchi kwani Watanzania wanawategemea wao kupanga mipango itakayoiletea nchi maendeleao lakini badala yake wanaingia bungeni wamelewa ilihali wizara yake inawasilisha bajeti.
Aidha kiongozi huyo amemtaka Rais Magufuli kuendelea na mapambano ya kuondoa umaskini unaoonekana kuwakandamiza Watanzania kwa kiasi kikubwa na njia pekee ya kuwakomboa ni kutengeneza mazingira ya kuwapatia ajira na kuboresha mazingira ya kilimo na biashara ili vijana wengi waweze kujiajiri.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts