SABABU YA MTANDAO WA WHATSAPP KUZIMWA NCHINI BRAZIL | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

5/6/16

SABABU YA MTANDAO WA WHATSAPP KUZIMWA NCHINI BRAZIL

 whatsapp

Mahakama ya Brazil imetoa amri ya kufungwa kwa Whatsapp kwa muda wa saa 72 (03/05/2016- 05/ 05/ 2016) baada ya Facebook, ambayo inamiliki mtandao huo kukataa kukabidhi taarifa ya mtu mmoja anayeshukiwa kuwa mlanguzi wa madawa ya kulevya.

Kwa mujibu wa habari kutoka Mashirika ya Habari ya Brazil ni kuwa walanguzi wa madawa ya kulevya nchini humo hutumia mtandao wa Whatsapp kujadili biashara hiyo haramu.

Hii ni mara ya pili ambapo Mahakama ya Brazil inatoa amri ya kufungwa kwa mtandao huo, mara ya kwanza Whatsapp ilifungwa kwa muda wa miezi sita.

Credit: trt

google+

linkedin