5/4/16

Sasa ni kutafuta Heshima sio Ubingwa-Mayanja

KOCHA wa Simba, Jackson Mayanja amesema pamoja na kupoteza matumaini ya ubingwa, lakini watajitahidi kuweka heshima kwa kushinda mechi zote zilizosalia.

Simba ilizidi kupoteza mwelekeo wa kutwaa ubingwa baada ya kutoka sare ya bila kufungana dhidi ya Azam katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.

Sare hiyo imefanya Simba kubaki nafasi ya tatu ikiwa na pointi 58, huku Azam ikiwa ya pili na pointi 59 nyuma ya Yanga inayoongoza ligi hiyo.

Akizungumza jana, Mayanja alikiri kupoteza mwelekeo baada ya sare na Azam, lakini anaamini ushindi wa mechi zilizosalia utaipa timu yake heshima.

“Ni kweli kabisa ile sare yetu na Azam iliharibu hesabu zetu, lakini huo ndio mpira wa miguu ulivyo, kila timu inahitaji ushindi kwa mechi za sasa… tunajipanga kushinda mechi zetu zote zilizosalia,” alisema.

Simba inatarajiwa kucheza na Mwadui kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, mechi ambayo itakuwa ya vuta nikuvute kutokana na timu hiyo kusheheni wachezaji wengi wazoefu waliopita timu mbalimbali za Ligi Kuu ikiwemo Simba.

Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts