5/3/16

Saudia imetekeleza adhabu ya kifo kwa watu 90 tangu mwanzoni mwa mwaka huu

Saudi Arabia imetekeleza adhabu ya kifo kwa watu 90 nchini humo tangu kuanza mwaka huu wa 2016.

Ripoti zinaonesha kuwa, idadi ya watu wanaouawa nchini Saudia baada ya kuhukumiwa adhabu ya kifo imeongezeka mno ambapo katika kipindi cha miezi minne iliyopita pekee watu 90 wametekelezewa adhabu hiyo.

Takwimu hizo zinaonesha kuwa, Januari Pili mwaka huu Saudia ilitoa hukumu ya adhabu ya kifo kwa wafuasi 47 wa madhehebu ya Shia kwa kosa la kuupinga utawala wa kifalme wa nchi hiyo ambapo hatua hiyo ni uvunjaji wa rekodi.

Mwaka uliopita pia Saudi Arabia ilitekeleza adhabu ya kifo dhidi ya watu 153, idadi ambayo haijawahi kushuhudiwa nchini humo katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.

Vitendo vya serikali ya Saudia vya kuwauwa raia kwa kisingizio cha upinzani dhidi ya watawala vinaendelea katika hali ambayo, mashirika mbalimbali ya kutetea haki za binadamu ulimwenguni yamekemea mara kadhaa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vinavyofanyika nchini humo.

Ripoti za asasi za kutetea haki za binadamu zinasema kuwa, nusu ya waliouawa baada ya kuhukumiwa adhabu ya kifo ni raia ambao walituhumiwa kufanya makosa ambayo si ya utumiaji mabavu. Hivi karibuni Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International lilitangaza kuwa, Saudi Arabia haifuati sheria za kimataifa na wala haiheshimu haki za raia wake.
 
chanzo: http://parstoday.com
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts