Contact us: yuvinusm45@gmail.com | email: yuvinusm45@gmail.com

We're Coming Soon

Tutarudi Baada ya Matengenezo

Tupo kwenye matengenezo ya Mtandao Wetu Tutarudi Mchakato Ukishakamilika, Tunaomba Radhi kwa Usumbufu Utakaojitokeza!

We are working very hard on the new version of our site. It will bring a lot of new features. Stay tuned!


days

hours

minutes

seconds

Subscribe to our newsletter

Sign up now to our newsletter and you'll be one of the first to know when the site is ready:

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger
Design by Yuvinusm

5/24/16

Serikali Imetenga Bilioni Nne Kujenga Nyumba za Walimu

 

Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni nne kwa ajili ya kujenga nyumba za walimu kwenye shule za msingi 40 katika wilaya 40 hapa nchini lengo likiwa kupatia ufumbuzi changamoto ya baadhi walimu kukataa kuripoti kwenye vituo vya kazi wanavyopangiwa kwa madai ya kukosekana kwa  miundoimbinu rafiki katika shule husika .

Akiongea na Waandishi wa Habari juu ya  miradi ya ujenzi wa nyumba hizo za walimu ambazo zitakua zinabeba familia sita kwa kila nyumba zikiwa na umeme wa jua na runinga, Meneja wa Mawasilaiano na Uhusiano  Mamlaka ya Elimu Tanzania Sylvian Lupembe amesema ujenzi huo utakamilika ndani ya mwaka huu ili kuongeza ufanisi kwa walimu na ufaulu kwa wanafunzi.

Kaimu Afisa Elimu Msingi kutoka  Halmashauri ya Mpwapwa Alexander Kiohi amesema mbali na kuwepo kwa tatizo la walimu lakini baadhi ya shule walimu wamekua wakigoma kwenda kuripoti kutokana na kukosekana kwa miundo rafiki huku mwalimu mkuu wa shule ya msingi mbuga Omary Mbwana ambapo  ujenzi wa nyumba hiyo unafanyika  amesema eneo hilo halina hata nyumba za kupanga ili walimu waweze kuripoti shuleni hapo.