5/2/16

Serikali Kulipa Madeni ya Walimu ya Waliohakikiwa tu

 

WAZIRI wa Fedha na Mipango Dokta Philip Mpango, ameliambia Bunge mjini DODOMA,  kuwa serikali inaendelea kuhakiki madeni ya walimu yaliyowasilishwa kwa ajili ya malipo baada ya kubaini kuwepo kwa udanganyifu kwenye baadhi ya madai hayo.Waziri Mpango amesema kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2015/2016, serikali ilipokea madai yenye jumla ya shilingi Bilioni 29 na Milioni 800 na imelipa shilingi Bilioni 20.125, huku madai mengine yakizuiwa baada ya kubainika hayakuwa halali.

Alitolea mfano wa mtumishi mmoja aliyewasilisha madai ya shilingi Milioni 600 badala ya shilingi laki 6, huku madai mengine yaliyolipwa miaka ya nyuma yakiwasilishwa kama madeni mapya.

Dokta Mpango amesema kuwa serikali inathamini mchango wa walimu katika maendeleo ya sekta ya elimu nchini na kwamba itaendelea kulipa madai yaona watumishi wengine wa umma baada ya kuyachambua, kuyahakiki na kujiridhisha kuwa ni halali.

Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm