5/12/16

Serikali kutoa 100,000/- atakayeonyesha shamba la bangi


SERIKALI mkoani Mara imeahidi kutoa zawadi ya Sh. 100,000 kwa kila atakayetoa taarifa ya kuwapo kwa shamba la bangi na wenyeviti wa serikali za vijiji na watendaji wao kupigwa faini ya Sh. 100,000 iwapo shamba litakutwa kwenye maeneo yao.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo, akizungumza wilayani Bunda jana kwenye mikutano ya hadhara, alisema lengo la hatua hiyo ni kutaka kukomesha kilimo cha zao hilo mkoani humo.
“Tutatoa kiasi hicho cha pesa kwa kila mwananchi ambaye atatuonyesha lilipo shamba la bangi,” alisema.
Aidha, alisema pia msako mkali wa kusaka watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria, utaanza wakati wowote baada ya siku 30 zilizotolewa na serikali za watu kuzisalimisha na kuhakiki silaha zao kumalizika.
Aliwataka wananchi wote kushirikiana na serikali pamoja na jeshi la polisi kuhakikisha vitendo vya uhalifu, ukiwamo ujambazi wa kutumia silaha unaisha mkoani hapa.
Pia aliliagiza jeshi la polisi mkoani hapa kupokeaa kesi za msingi tu kwenye vituo vyao zinazohusu jinai, huku zile za kudaiana wao kwa wao kutakiwa kwenda wenyewe mahakamani kufungua kesi za madai na wala si kumweka mdaiwa mahabusu kwa kukopesha wao kwa wao.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts