5/6/16

Serikali Yairejeshea Usajili Taasisi ya Kimataifa


WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imerejesha usajili wa taasisi ya ya kimataifa ya African Wildlife Foundation (AWF) ilioufutwa katika daftari la usajili Machi mwaka huu.
Mkurungenzi wa AWF, John Salehe.
Mkurungenzi wa AWF, John Salehe, alisema jijini hapa jana kuwa serikali imeirejesha taasisi hiyo Aprili 21, mwaka huu, katika daftari la usajili.
AWF ilikuwa ni miongoni mwa asasi 110 ambazo usajili wake ulifutwa Machi, mwaka huu kwa madai ya kutowasilisha taarifa za mwaka katika kipindi cha miaka miwili na kushindwa kulipa kulipa kodi.
Salehe alisema taasisi yake inayojishughulisha na masuala ya uhifadhi wa wanyamapori na sasa hivi miradi ya kuwawezesha wananchi kuhusu kilimo na mradi wa mbwa maalumu wanaodhibiti majangili, ilikwisha timiza masharti hayo, lakini kwa bahati mbaya kumbukumbu hizo hazikuonekana upande wa wizara.
Hata hivyo, alisema walilazimika kulipa tena, ingawa baadaye risiti za awali zilionekana.
Katika barua ya kurejesha usajili ya Aprili 21 kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya kwenda kwa Mkurungezi wa AWF nchini, ilisema katika kikao chake cha Aprili 19, mwaka huu, Bodi ya NGOs ilipitisha uamuzi wa kuirejesha taasisi hiyo katika daftari la usajili.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm