5/2/16

Sherehe za Harusi, Misiba Korea Kaskazini ni Marufuku

Rais Kim Jong-un wa Korea Kaskazini, amepiga marufuku sherehe za misiba na harusi nchini humo, wiki moja kabla ya hafla yake ya kuvikwa taji na chama chake la kuwa Kiongozi Mkuu nchini humo.
Imeripotiwa kuwa Korea ya Kaskazini imeimarisha usalama katika Mji Mkuu wake Pyongyang, ili kuepuka maafa yoyote katika tukio hilo. Duru za siasa nchini humo zinaripoti kuwa hafla hiyo hufanywa mara chache na chama hicho tawala hivyo upekee wa shughuli hiyo ndio umefanya Rais Kim kupiga marufuku sherehe hizo.
Mbali na kuzifungia sherehe za harusi na huduma za mazishi kwa wiki hii kwa sababu za kiusalama , kwa mujibu wa Times Jumapili; Korea ya Kaskazini katika siku za nyuma imewahi kuchukua hatua kama hiyo kwa kuufunga mpaka wake na China, katika matukio makubwa kama hayo.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 33 katika hotuba yake anatarijwa kutoa muongozo wa mustakabali wa taifa hilo kuhusu hali ya silaha za nyuklia wa miaka 36 katika mkutano wa kwanza.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm