5/9/16

Shetta Ataja Kolabo Zake Za Kimataifa

 

Muziki wa kizazi kipya hapa Tanzania ulianza miaka ya 1990 na ina semekana Mr 2 Sugu ndiye muanzilishi na wakati huo ilionekana kama uhuni, kwa sasa wanaofanya muziki huo ndio wanaopiga pesa nyingi; wasanii kama kina Ali Kiba, Diamond Platnumz na Ommy Dimpoz wameng’ara na kupata mafanikoa kutokana na kazi za muziki, Je Shetta kwa upande wake inasemaje?

SHETTA ANA MIPANGO GANI ?

Baada ya kutoa ngoma yake mpya inayoenda kwa jina la ‘Hamjui’ huki ikifanya vizuri katika vituo mbalimbali vya Radio na Tv. Shetta amesema ana “Project” na wasanii kadha wa kadha akiwemo Roberto aliyeimba Amarula na wasanii wengine.

“Nina project na Roberto aliyeimba Amarula nina project na wasanii wa Zambia, Kenya na Uganda pia miongoni mwa hizo project kuna ambazo tumefanya yoyote anaweza kuitumia katika project binafsi” amesema Shetta.

Shetta alitoa ngoma ya Shikorobo aliyomshirikisha Kcee kisha akasimama kwa muda mrefu ndipo sasa akaibuka na kibao kipya kilichotoka mwishoni mwa wiki huku akisisitiza kuna Collabo nyingi za kimataifa anazotazamia kuzifanya na zikikamilika  ataweka wazi.

Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm