5/9/16

Simba Yavunja Timu Nzima ...Sababu Iko Hapa

Mashabiki wa Simba 

KOCHA pekee raia wa Uganda kwenye Ligi Kuu ya Bara, Jackson Mayanja anataka kuandika historia. Kama alichopanga kukifanya kikikubalika na vigogo wa klabu yake ya Simba huenda akaingia kwenye rekodi.

KOCHA pekee raia wa Uganda kwenye Ligi Kuu ya Bara, Jackson Mayanja anataka kuandika historia. Kama alichopanga kukifanya kikikubalika na vigogo wa klabu yake ya Simba huenda akaingia kwenye rekodi.
Mayanja maarufu kama Miamia nchini kwao, amewashtua viongozi baada ya kuwaambia kwamba anataka kubakiwa na wachezaji watano tu kwenye kikosi cha sasa cha Simba.
Hiyo inamaanisha kwamba viongozi kama wakikubali masharti yake na kubaki naye, watalazimika kupukutisha wachezaji 20 katika kikosi cha sasa na kubakiwa na watano tu ambao kikanuni hawatoshi kuunda kikosi cha kushindana uwanjani.
Habari za ndani ambazo Mwanaspoti imezipata jana kutokana kwa mmoja wa vigogo nyeti kwenye kamati ya usajili ya Simba ni kwamba Mayanja amependekeza yafanyike maamuzi magumu kuinusuru timu ambayo imepoteza hadhi ya kimashindano kimataifa.
“Wengi wameshtuka, yeye anataka abaki na wachezaji watano tu kwenye kikosi hiki cha sasa. Amejaribu kujenga hoja kwamba wachezaji wengi hawajitumi kwaajili ya klabu, hawana uwezo wa kuirejesha Simba kwenye chati yake ndio maana imekuwa ikirudi palepale kila mwaka.
“Anadai kwamba kuna Wachezaji miungu watu ambao wamezoea kudekezwa na viongozi na wanafanya mambo wanavyotaka, hilo yeye halitaki. Anasisitiza kwamba anataka kutengeneza timu yake mpya kabisa akiwa na msaidizi wake. Wachezaji anaotaka kubaki nao wamefanya kazi kubwa sana msimu huu, lakini hawa 20 ni wengi sana,”alidokeza kigogo huyo.
Lakini aligoma kuweka wazi orodha ya majina hayo matano au yale 20 ya anaotaka waondoke kwa madai kwamba bado hawajaafikiana naye na yakitajwa kwasasa huenda yakatibua mambo na timu ikapoteza hata mechi zilizobaki.
Habari zinasema kwamba Mayanja mwenye misimamo mikali amewaambia endapo watashindwa kumtekelezea majukumu hayo hatakuwa tayari kuendelea na Simba kwavile hataki kuwa na nidhamu ya woga ambayo itakuja kumchafulia heshima yake siku zijazo.
Rais wa Simba, Evans Aveva jana Jumapili hakutoa ushirikiano, lakini kwenye gazeti hili toleo lililopita alisisitiza kwamba kuna mabadiliko makubwa yanakuja ndani ya Simba na kwamba anaelewa uchungu wanaopata mashabiki na wanachama pale timu hiyo inapopoteza mechi.
Kocha huyo inaelezwa kuwa amewaambia viongozi waziwazi kwamba wakiendelea na aina hiyo ya wachezaji waliopo klabuni kwasasa ni ngumu kufika popote ingawa kauli hiyo imepingwa na baadhi ya vigogo kwa madai kwamba mbona kwenye mechi za awali walikuwa wakijituma?
Mayanja alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusiana na hilo alijibu kwa kifupi kwamba; “Huu siyo wakati muafaka ngoja tumalize ligi.”
Habari za ndani zinadai kwamba Mayanja amekuwa akipingwa na baadhi ya viongozi kutokana na misimamo yake ambapo wamekuwa wakimsihi apotezee baadhi ya vitendo vya wachezaji lakini amekuwa akigoma na kusimamia nidhamu
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts