5/9/16

Sitta alaani udhalilishaji wabunge wanawake

 Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge Wanawake
Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge Wanawake Bungeni, Margaret Sitta amesema kitendo cha wabunge kutumia maneno ya kuudhi, kudhalilisha na kukashfu Bungeni hakikubaliki na ni kinyume cha katiba na kanuni za Bunge.
Akitoa hoja binafsi leo bungeni, Sitta ambaye ni mbunge wa Urambo Mashariki kupinga kauli ya unyanyasaji iliyojitokeza wiki iliyopita na kuwafanya wabunge wanawake wa kambi ya upinzani kutolewa nje ya Bunge, Sitta amesema kauli hizo si tu zinawazalilisha wanawake bali  zinapungza heshima ya chombo hicho.
Amesema pamoja na Naibu Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson kuamuru maneno ya udhalilishaji dhidi ya wanawake kufutwa kwenye kumbukumbu za Bunge, vitendo vyovyote vinavyotoa harufu ya udhalilishaji wa kijinsia bungeni havikubaliki.

Mwananchi
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts