5/3/16

Taarifa kwa Wanachama wa Tanzania Bloggers Network (TBN)

Chama cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Jamii nchini ‘Tanzania Bloggers Network’ – TBN inawaomba wanachama wake wote kutotumia taarifa ama habari au picha yoyote kutoka katika mkutano wa maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari unaofanyika kitaifa mkoani Mwanza.
Kamati Kuu ya Uongozi TBN imefikia hatua hiyo leo baada ya kujadiliana na kujiridhisha kuwa kumekuwepo na taasisi ambazo zimekuwa zikiwatenga wanahabari wa mitandao ya kijamii (bloggers) na kutotambua umuhimu wao wakati sehemu kubwa ya taarifa mbalimbali nchini usambazwa na mitandao hiyo.
TBN iliyosajiliwa rasmi serikalini Aprili 2015 na kupewa namba ya usajili; S. A 20008 inaendelea kuwataarifu wanachama wake kuendelea kutotoa ushirikiano kwa taasisi ambazo zinaonekana kuwatenga bloggers na kutotambua mchango wao.
Imetolewa na;- Mwenyekiti wa Muda wa TBN
Joachim E. Mushi
03/05/2016
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts