5/7/16

TFF YAFAFANUA UWAKILISHI WA VILABU KIMATAIFA

YANGA NA AZAM

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa ufafanuzi juu ya nafasi ya  uwakilishi wa Vilabu Kimataifa. Bingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa msimu 2015/16 inayoendelea kama atashinda pia taji katika fainali ya Kombe la Shirikisho maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), ndiye atayeiwakilisha nchi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika msimu wa 2016/17.

Kwa msingi huo, timu ambayo itafungwa katika fainali hiyo ya Kombe la Shirikisho – ASFC linalodhaminiwa na Kituo cha Televisheni cha Azam, ndiyo itakayowakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika katika msimu wa 2016/17.

Fainali ya Kombe la Shirikisho kati ya Yanga na Azam inatarajiwa kufanyika baadaye mwezi ujao, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya mchuano uliohusisha timu 64 za Ligi Kuu Tanzania Bara – VPL (16); Ligi Daraja la Kwanza -FDL (24), na Ligi Daraja la Pili – SDL (24).

Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts