5/11/16

TUHUMA MPYA: LABDA HII NDIYO SABABU YA AJIB KUJIPATISHA KADI NYEKUNDU


Mshambuliaji Ibrahim Ajib wa Simba ametimkia nchini Afrika Kusini. Taarifa zinaeleza, Ajib anakwenda kufanya majaribio katika timu ya Orlando Pirates lakini uongozi wa Simba, haukuridhia.
Kutoka ndani ya Simba, taarifa zinaeleza Ajib aliomba ruhusa kwenda Afrika Kusini kupitia mtu aitwaye Ndambile mara baada ya mechi dhidi ya Mwadui FC.
“Sasa hiyo ikashangaza sana, kweli mtu anakwenda majaribio anaweza kuomba ruhusa saa chache kabla ya kuondoka.
“Kwani majaribio ni suala la kushitukiza, hakika imewashangaza sana viongozi na hawakutoa ruhusa lakini ameondoka.
“Hii inaanza sasa kuhusisha na ile kadi nyekundu aliyepata katika mechi dhidi ya Mwadui. Maana haikuwa na sababu, sasa alifanyaje hivyo, au ndiyo alitaka apate nafasi ya kwenda Afrika Kusini?” kilieleza chanzo.
Ajib ni kati ya wachezaji waliokulia Simba kisoka na amepata mafanikio mwanzoni au katikati ya msimu. Lakini mwishoni ameonekana kupungua makali
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm