5/4/16

Tulipiga hela CCM, wakatuonea wivu - Nyauloso


Msanii Nyauloso amefunguka juu ya kile kilichotokea baada ya kuisha kwa kampeni za urais ambazo Rais Dkt. John Magufuli aliibuka mshindi.
Msanii huyo ambaye alikuwa miongoni mwa wasanii waliokuwa wakiipigia kampeni CCM chama ambacho kipo madarakani, alisema ingawa walipata hela nzuri, lakini walipata tabu sana kipindi hicho cha kampeni kutoka kwa jamii na wasanii wenzao, lakini baadaye walikuja kujuta na kutamani nao wangeipigia kampeni CCM.
"Tumepata mkwanja mrefu kwa kweli, na tulikuwa tunapata shida ila baada ya Dkt. Magufuli kutangazwa mshindi tukapongezwa, wengine wakawa wanasema bora nyinyi mlikuwa huku, yani mpunga tulichukua wa uhakika," alisema Nyauloso akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio.
Mwaka jana kipindi cha kampeni kulikuwa na mvutano mkubwa kwa wasanii waliokuwa wakipigia kampeni vyama vya siasa, huku wengi wakilaumiwa kufanya hivyo kutokana na njaa ya pesa, na sio mapenzi ya dhati kwa chama husika.

-EATV
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts