Contact us: yuvinusm45@gmail.com | email: yuvinusm45@gmail.com

We're Coming Soon

Tutarudi Baada ya Matengenezo

Tupo kwenye matengenezo ya Mtandao Wetu Tutarudi Mchakato Ukishakamilika, Tunaomba Radhi kwa Usumbufu Utakaojitokeza!

We are working very hard on the new version of our site. It will bring a lot of new features. Stay tuned!


days

hours

minutes

seconds

Subscribe to our newsletter

Sign up now to our newsletter and you'll be one of the first to know when the site is ready:

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger
Design by Yuvinusm

5/17/16

Ujenzi wa Reli ya Rwanda-Bandari ya Dar Kukamilika 2018

reli ya rwanda - tz

Aprili 23 mwaka huu Tanzania ilitangazwa rasmi kuwa na uhalali wa kujenga bomba la kusafirisha mafuta gafi kutoka Uganda kupitia Bandari ya Tanga mara baada ya Rais wa Uganda Yoweri Museven kukutana na Rais Magufuli wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Arusha.

Siku chache baadaye Tanzania ilipata dili jingine kutoka Uganda la kujenga bomba jingine jipya la gesi katika njia hiyohiyo kwa lengo la kufanya biashara na Tanzania, katika kuthibitisha ule usemi usemao aliyenacho anaongezewa mara dufu safari hii sio Uganda tena bali Tanzania imepata fursa nyingine kiuchumi baada Rwanda kutangaza mpango wa kujenga reli inayoungana na Bahari ya Hindi kupitia Bandari ya Dar es Salaam, kwa kile kilichodaiwa chaguo hilo ni la gharama ya chini na umbali mfupi ikilinganshwa na mpango wa kupitia Kenya.

Mwaka 2013 Rwanda, Kenya na Uganda zilikubaliana kujenga reli itakayoungana na Bandari ya Mombasa kwa gharama ya dola bilioni 13 ambayo ingeigharimu Rwanda dola bilioni moja za kimarekani, utafiti uliofanywa na nchi sita wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaonesha kuwa chaguo la Tanzania litaigharimu Rwanda kati ya dola milioni 700 na 800.

Waziri wa Fedha wa Rwanda Claver Gatete amesema mbali na ukaribu ujenzi wa reli hiyo hautachukua muda mrefu na unatarajiwa kukamilika Machi 2018.