Contact us: yuvinusm45@gmail.com | email: yuvinusm45@gmail.com

We're Coming Soon

Tutarudi Baada ya Matengenezo

Tupo kwenye matengenezo ya Mtandao Wetu Tutarudi Mchakato Ukishakamilika, Tunaomba Radhi kwa Usumbufu Utakaojitokeza!

We are working very hard on the new version of our site. It will bring a lot of new features. Stay tuned!


days

hours

minutes

seconds

Subscribe to our newsletter

Sign up now to our newsletter and you'll be one of the first to know when the site is ready:

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger
Design by Yuvinusm

5/13/16

Ukawa Waipa Talaka CCM

WABUNGE 53 wanaotoka kwenye vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wametengana rasmi na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kujiondoa kwenye Umoja wa Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG).


Hatua hiyo inakuja baada ya Goodluck Mlinga, Mbunge wa Ulanga (CCM) hivi karibuni kudai kwamba, anayeteuliwa kuwa mbunge wa viti maalum ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) lazima aitwe ‘beby’ ikiwa na maana ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi.

Kwa mujibu wa barua ya kujitoa iliyotolewa 6 Mei yenye saini 53 za wabunge hao 53 na kunakiliwa kwa Job Ndugai, Spika wa Bunge, wabunge hao wamesema;

“Licha ya juhudi mbalimbali zilizofanywa na wabunge wa upinzani kutaka mwongozo wa spika ili Mlinga afute kauli yake, Naibu Spika (Dk. Tulia Ackson) alipuuza miongozo hiyo.”

Wamesema kauli hiyo imewadhalilisha kama wanawake na pia wabunge wa upinzani.

Juzi Lilian Liundi, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) alilaani vikali kitendo cha udhalilishwaji na matumizi ya lugha chafu na za kejeli dhidi ya wanawake bungeni na kwamba, kilichotokea bungeni ni muendelezo wa matukio ya utumiaji wa lugha ya kudhalilisha jambo ambalo halivumiliki.