Contact us: yuvinusm45@gmail.com | email: yuvinusm45@gmail.com

We're Coming Soon

Tutarudi Baada ya Matengenezo

Tupo kwenye matengenezo ya Mtandao Wetu Tutarudi Mchakato Ukishakamilika, Tunaomba Radhi kwa Usumbufu Utakaojitokeza!

We are working very hard on the new version of our site. It will bring a lot of new features. Stay tuned!


days

hours

minutes

seconds

Subscribe to our newsletter

Sign up now to our newsletter and you'll be one of the first to know when the site is ready:

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger
Design by Yuvinusm

5/18/16

Ukawa walizidi Bunge Maarifa


WAKATI juzi Kamati ya Kanuni za Bunge ilizuia kuwasilishwa kwa taarifa ya maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,

Iliyoelezwa kusheheni ukiukwaji Kanuni za Kudumu za Bunge, Kambi hiyo jana iliirejesha 'kiana' taarifa hiyo bungeni mjini hapa.

Kabla ya kuwasilishwa kwa hotuba ya makadirio ya bajeti ya wizara hiyo juzi asubuhi, Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan 'Zungu', alimwagiza Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Godbless Lema, kukutana na Kamati ya Kanuni ili kujadiliana kuhusu maudhui yaliyokuwamo kwenye taarifa yake.

Baadaye jioni, Zungu alimtaka Lema kufuta baadhi ya vipengele vilivyokuwamo kwenye taarifa yake ili ikidhi matakwa ya Kanuni za Bunge, lakini Mbunge huyo wa Arusha Mjini (Chadema), akaamua kutoisoma taarifa hiyo bungeni kwa kile alichoeleza kuwa agizo la Zungu lilimaanisha taarifa yake yote ifutwe.

Kabla ya kutoa agizo hilo, Zungu alivitaja vipengele vya taarifa ya Lema vilivyokuwa vinakiuka Kanuni za Kudumu za Bunge kuwa ni pamoja na 'mauaji ya viongozi wa kisiasa', mkataba tata kati ya Kampuni ya Lugumi na Jeshi ya Polisi' na 'kuuzwa kwa nyumba za serikali'.

Vingine ni 'rushwa na bunge kutumika kulinda wahalifu pamoja na kumzungumzia Rais John Magufuli na usalama wa nchi'.

Hata hivyo, ya licha kuzuiwa kuwasilisha bungeni juzi, jana asubuhi, Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, James Mbatia alizungumzia baadhi ya vipengele alivyokatazwa Lema wakati akiwasilisha taarifa yake bungeni.

Mbatia alizungumza masuala karibu yote ambayo Lema alizuiwa kuyazungumza juzi katika lugha isiyokuwa kali ingawa alimwaga tuhuma nyingi dhidi ya serikali.

Na alipotafutwa na Nipashe kwenye viunga vya Bunge jana mchana, Mbatia alikiri kuwasilisha bungeni sehemu ya taarifa ya Lema ingawa alidai kwa lugha isiyo kali.

"Kwenye hotuba yangu ya leo (jana) nimeyarudia baadhi ya mambo ambayo Lema alizuiwa kuyasema bungeni kutokana na umuhimu wake kwa taifa," alisema Mbatia.

Baadhi ya vipengele vilivyowasilishwa na mbunge huyo ni pamoja na vile vilivyozungumzia kuwepo kwa utawala wa kiimla na kidikteta, uuzwaji wa nyumba za serikali, ubovu wa miundombinu na hasara ya mabilioni katika Wakala wa Barabara nchini (Tanroad).

UTAWALA WA KIIMLA
Mbatia alisema Sheria ya Makosa ya Mtandao Na. 14 ya mwaka 2015, ilipingwa na Kambi ya Upinzani, lakini ikapitishwa na wabunge wa chama tawala na kwamba zipo dalili sheria hiyo kandamizi ilitungwa kwa shinikizo la chama tawala kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka jana kutokana na kasi ya vijana ambao wengi wao walikuwa wanaunga mkono upinzani.

"Baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu, ushahidi unaonyesha sheria hiyo mbaya ilitungwa kwa makusudi ya kuwabana Watanzania ambao wapo tayari kuukosoa utendaji mbovu wa serikali ya awamu ya tano kwa kuleta utawala wa kiimla na kidikteta," alisema Mbatia.

Alisema kitendo cha Shirika la Changamoto za Milenia la Marekani (MCC) kuiondoa Tanzania kama mnufaika wa misaada yake, kinatokana na tamko la bodi ya wakurugenzi wa MCC iliyotolewa Machi 28, mwaka huu kuwa mojawapo ya sababu za kuondolewa ni uwapo wa sheria hiyo.

NYUMBA ZA SERIKALI ZILIZOUZWA
Mbatia alisema kati ya mwaka 2002 na 2004, serikali iliuza nyumba 7,921 na mpaka mwaka 2008, ilikuwa imejenga nyumba 650 tu.

Alisema katika biashara hiyo ya kuuza nyumba zilizokuwa mali ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), ilipata Sh. milioni 252.603 na sasa inahitaji kusaka nyumba zaidi ya maradufu ya kiasi hicho kujenga nyumba za fidia.

"Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza waliouziwa nyumba hizo kinyume cha mikataba ya mauzo, wanyang'anywe," alisema na kuongeza:

"Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka serikali kutekeleza azimio la Bunge la Aprili 25, 2008 kuzirejesha nyumba hizo, na kwa njia hiyo ile kaulimbiu ya 'Hapa Kazi Tu', iweze kutafsiriwa kwa vitendo.

HASARA SH. BIL 5.6 TANROADS
Aidha, Mbatia alisema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), amebaini Tanroads ina utendaji mbovu ikiwa ni pamoja na usimamiaji wa mikataba ya ujenzi wa barabara na madaraja.

Mbatia alisema Tanroads imetia hasara ya Sh. bilioni 5.616 kutoka kwenye riba inayoongezeka kila siku kutokana na wakala huyo kutowalipa makandarasi 11 katika kipindi cha mwaka 2012 hadi 2015.

UFISADI UPANUZI JNIA
Mbatia pia, alisema upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) katika kituo cha tatu (Terminal Three) ulikuwa na harufu ya ufisadi.

"Kuna tuhuma kwamba mtu ambaye alikuwa ni dalali katika mchakato mzima wa Tanzania kupatiwa mkopo wa ujenzi wa uwanja huo, alifanikiwa kupata asilimia 30 ya mkopo kama kamisheni yake inayofikia Dola za Marekani milioni 100, zaidi ya Sh. bilioni 200 za Tanzania.

Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka serikali kuliangalia suala hili kwa undani na kuleta taarifa hapa bungeni, au kwenye kamati husika ya Bunge," alisema.

UFISADI VIVUKO, MADARAJA
Mbunge huyo wa Vunjo (NCCR), alisema kivuko kutoka Dar es Salaam kwenda Bagamoyo ni jipu ambalo limeiva kwa viwango vyote na sasa linatakiwa kutumbuliwa mara moja.
Alisema kivuko hicho kilichonunuliwa na Wakala wa Karakana ya Magari na Umeme wa Serikali (Temesa).

"CAG alibaini ununuzi wa boti feki na mbovu uliofanywa na Temesa na kugharimu Dola za Marekani milioni 4,980, sawa na Sh. bilioni 7.916 kupitia mkataba namba AE/006/2012-13/HQ/G/CN-39 uliosainiwa Aprili 21, 2013 kati ya Temesa kwa niaba ya serikali na mzabuni M/s Johs.Gram-Hanssen Bergensgade," alisema na kuongeza:

"CAG alibaini masuala makuu mawili, kuhusu ununuzi huo wa kivuko feki na kibovu cha Dar es Salaam - Bagamoyo.

Jambo la kwanza CAG alibaini kasi ya kivuko hicho ni tofauti na kasi iliyotakiwa kuwapo, jambo la pili ni kuwa cheti cha kukikubali kivuko hicho kilikuwa hakijatolewa, kinyume cha Kanuni ya 247 ya Manunuzi ya Umma.

HALI YA RELI NCHINI
Mbatia alisema ujenzi wa reli kwa kiwango cha 'standard gauge' uende sambaamba na kuimarisha mawasiliano katika kuendesha shughuli za reli ili kuongeza ufanisi.

BAJETI YA WIZARA
Akiwasilisha hotuba ya makadirio ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka ujao wa fedha, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, alisema kuwa wizara hiyo inahitaji Sh. trilioni 4.895 ili kutekeleza majukumu yake. Kiasi hicho cha fedha ni sawa na asilimia 41.4 ya bajeti yote ya taifa ya maendeleo mwaka 2016/17 ambayo ni Sh. trilioni 11.82.

Kati ya Sh. trilioni 4.895 zilizoombwa na Prof. Mbarawa, Sh. trilioni 2.212 ni kwa ajili ya Sekta ya Ujenzi, Sh. trilioni 2.587 ni kwa ajili ya Sekta ya Uchukuzi, wakati Sekta ya Mawasiliano imeombewa Sh. bilioni 95.804.