5/9/16

Utabiri wa Profesa Jay Kwa Wasanii wa HipHop TZ

 

Kuna majina ukiyasikia katika tasnia ya muziki hapa Tanzania unaweza ukawa unafurahi mwenyewe bila hata ya kuambiwa ufurahi, uzuri wake hicho anacho kiimba ndicho anakifanyia kazi kwa sasa. unaweza kufikiri ninani huyo? jibu Joseph Haule a.k.a Profesa Jay ambaye hivi sasa ni Mbunge wa Jimbo la Mikumi.

PROFESA JAY NI NANI?

Profesa Jay amefanya makubwa katika muziki wa Tanzania pengine nyimbo zake alizokuwa anatunga ndizo zilizomfanya ajiamini na kujitosa katika siasa, hivi unakumbuka kibao kilichoitwa Ndiyo Mzee? Kikao cha Dharura? Nang’atuka? zote hizo zilihusu siasa na watu walikuwa wanadhani siku moja atakuwa kingozi wa siasa na hatimae imekuwa kweli.

ATABIRI HAYA KWA WASANII WA HIPHOP

Prof. Jay amefunguka na kuwamwagia sifa wasanii wanaofanya muziki wa HipHop  kwa kazi nzuri walizo zifanya akiamini huenda wasanii hao wakawa na vitu vya ziada huku akitolea mifano ya mashairi kama ya wasanii  Kala Jeremiah, Roma, Nick wa pili na Mwana Fa .

“Wasanii wanamsimamo na wana shule kazi ya ubunge inatakiwa ujipange kwa ajili ya kuwatumikia wananchi, wasani hao wanavitu kulingana na mashairi yao labda tu bado wanahofia kushika peni na karatasi ushakuwa kiongozi” Maneno ya Profesa Jay.

Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts