5/5/16

Utaratibu wa Kuchukua Fomu Yanga Huu Hapa

 

Baada ya TFF kutangaza rasmi uchaguzi wa klabu ya Yanga kufanyika June 25 mwaka huu, timu hiyo imetangaza tarehe ambayo fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi zitaanza kutolewa.

Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit ameweka wazi tarehe ya kuchukua fomu ni Mei 27 wakati tarehe ya kurejesha ni Mei 29.

Baraka amesema baada ya zoezi hilo Kamati ya uchaguzi itaanza kusikiliza pingamizi zitakazokuwa zimewasilishwa huku orodha ya mwisho ya wagombea waliopitishwa ikitarajiwa kutangazwa Juni Mosi.

“Tunataka kwenda na muda ambao tumepangiwa na BMT na TFF, ndiyo maana mchakato huu tunauweka wazi kwa ajili ya Wanachama wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali waweze kuingia kwenye kuchukua fomu za kugombea,” amesema Baraka.

Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm