Contact us: yuvinusm45@gmail.com | email: yuvinusm45@gmail.com

We're Coming Soon

Tutarudi Baada ya Matengenezo

Tupo kwenye matengenezo ya Mtandao Wetu Tutarudi Mchakato Ukishakamilika, Tunaomba Radhi kwa Usumbufu Utakaojitokeza!

We are working very hard on the new version of our site. It will bring a lot of new features. Stay tuned!


days

hours

minutes

seconds

Subscribe to our newsletter

Sign up now to our newsletter and you'll be one of the first to know when the site is ready:

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger
Design by Yuvinusm

5/18/16

Uwanja wa Taifa kuubeba U/Uhuru


KATIKA kuhakikisha inaimarisha ulinzi na usalama viwanjani na kuongeza mapato, serikali imeagiza mashabiki wa soka watumie mageti ya Uwanja wa Taifa kuingia Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Katika mahojiano maalum na Nipashe kwenye viunga vya Bunge mjini hapa juzi, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Michezo katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Alex Mkenyenge, alisema utaratibu huo mpya utaanza rasmi msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Alisema serikali imetumia Sh. bilioni 10 kukarabati Uwanja wa Uhuru, lakini hauna mageti ya kutosha kuingiza mashabiki wa soka bila bughudha, hivyo wameona kuna haja ya kutumia milango ya Uwanja wa Taifa ambao una mageti mengi.

Uwanja wa Uhuru ulifungwa kutumika kwa mechi za soka mwanzoni mwa mwaka 2011 ili ukarabatiwe na Kampuni ya Beijing Construction ya China, unapakana na Uwanja wa Taifa.

"Ukarabati wa Uwanja wa Uhuru umekamilika na utaanza kutumika tena kwa mechi za soka msimu ujao," alisema Mkenyenge na kueleza zaidi:

"Kutokana na changamoto za kiusalama, tumeamua kuja na utaratibu mpya kwa mashabiki kuingia kwenye uwanja huo. Mashabiki sasa watakuwa wanatumia mageti ya Uwanja wa Taifa kabla ya kuingia Uhuru."

Alisema tayari wameshasimamia mfumo wa tiketi za kieletroniki kwenye milango ya Uwanja wa Taifa ili kuimarisha ukaguzi wa tiketi na kudhibiti uingiaji wa mashabiki uwanjani.

Mkenyenge aliendelea kueleza kuwa wakati wa mechi, mageti yaliyopo kwenye uzio unaotenganisha Uwanja wa Taifa na Uhuru yatakuwa yanafunguliwa kurahisisha uingiaji wa mashabiki na kwamba mageti manne ya Uhuru yatatumika tu kwa mashabiki wanaotoka uwanjani.

"Pale Taifa tayari tumesimika mfumo wa tiketi za kielektroniki. Uwanja wa Uhuru hauna mfumo huo wa kisasa. Na hata ukisimikwa, bado mashabiki watalazimika kupita kwenye milango ya Uwanja wa Taifa kwa sababu Uhuru kuna mageti manne tu," Mkurugenzi huyo alisema.

Kuhusu changamoto ya Uwanja wa Taifa kutokuwa na njia na eneo maalum la kuketisha waandishi wa habari, Mkenyenge alikiri maofisa wa serikali waliopitia michoro ya ujenzi wa uwanja huo, hawakulitilia mkazo suala hilo.

"Wakati tunaletewa michoro, hatukujua jambo hili la eneo la kukaa waandishi. Hatukuwa na uzoefu katika ujenzi wa viwanja vya kisasa maana hapo kabla hatukuwahi kujenga uwanja mkubwa kama huo (Uwanja wa Taifa)," alisema.

Aliongeza: "Kuna viwanja ambavyo vina hali mbaya zaidi. Uwanja wa CCM Kambarage pale Shinyanga, kwa mfano, una changamoto nyingi. Kuna watu wanaishi, wamepanga ndani ya uwanja huo."

Uamuzi huo wa serikali umetolewa ikiwa ni siku chache baada ya gazeti hili kuchapisha ripoti maalum iliyofichua namna viwanja vya soka nchini vilivyo hatari kwa usalama wa wachezaji na mashabiki kutokana na kutokuwa na miundombinu inayokidhi masharti ya usalama viwanjani.

Katika ripoti hiyo, Ofisi Usalama wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) nchini, Jonas Mahanga, aliweka wazi kuwa Tanzania haina hata uwanja mmoja wa soka unaokidhi matakwa ya Kanuni za Usalama za shirikisho hilo lenye mamlaka ya juu ya soka duniani.