5/10/16

VIDEO: ‘Hali ya ajira Tabora ni mbaya, vijana hawana ajira’ -Mbunge Munde Tambwe


Bunge limeendelea tena Dodoma, Wizara mbalimbali zimekuwa zikiwasilisha ripoti za makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2016/2017 huku Wabunge wakipata nafasi ya kuchangia maoni kabla ya kuzipitisha  katika bajeti.
Hapa nakukutanisha na Mbunge wa viti maalumu Tabora Munde Tambwe pale aliposimama bungeni kuchangia bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
>>’Nimkumbushe Waziri wa Viwanda na Biashara kuwa Tabora inalima tumbaku kwa asilimia 60, Serikali imewekeza sana kwenye Reli na Barabara hii pia inasaidia sisi kuwa na viwanda vingi lakini sioni sababu ya kutokuwa na viwanda hivyo hadi sasa
Hali ya ajira Tabora ni mbaya vijana hawana ajira., sijui ni nani alitoa wazo la kiwanda cha tumbaku kupelekwa Morogoro wakati tumbaku inalimwa Tabora kwa asilimia kubwa zaidi
Leo namuomba Waziri ageuze zao la asali kuwa zao la biashara, lakini pia tupate viwanda vya kutengeneza asali ili vijana wetu wafaidike na zao hili na tupunguze umaskini
Unaweza kuendelea kusikiliza kwenye hii video hapa chini…
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm