5/6/16

Vijana walaumiwa kuchagua ajira, uvivu

MKURUGENZI wa Idara ya Ajira Zanzibar, Ameir Ali Ameir, amesema tatizo la ajira nchini ni changamoto kubwa kwa vijana, kutokana na wengi wao kukosa sifa za kuajiriwa na baadhi yao kuchagua kazi.
Mkurugenzi wa Idara ya Ajira Zanzibar, Ameir Ali Ameir.

Amesema mtazamo wa baadhi ya vijana katika kufanyakazi ni tatizo na baadhi yao wamejenga tabia ya uvivu.

Alisema hayo wakati juzi akifungua mafunzo ya kuzijengea uwezo kamati za ajira za wilaya za Mjini na Magharibi, Zanzibar.

Alizitaka kamati hizo kujipanga vizuri na kuyafuatilia matatizo yanayowakabili vijana ili kuwanusuru kujiingiza katika
vikundi viovu.

“Ni kazi ya kamati kupita kwa waajiri ili kuangalia changamoto, mafanikio na utamaduni wa vijana na kufahamu matatizo yao kupitia vigezo vyao na kuona wazee wana nafasi gani katika kuwasaidia,” alisema.

Aidha, Ameir alizitaka kamati hizo kutafuta changamoto zinazosababisha vijana kukosa ajira ili kuwasaidia na kuwaingiza katika soko la ajira.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts