5/9/16

Vijana, wanawake kunufaika sekta za kilimo, utalii


 
 Zaidi ya vijana na wanawake 50,000 wanatarajiwa kunufaika na programu ya kujikwamua kiuchumi na kupata ajira kupitia sekta za kilimo na utalii nchini.
Makundi hayo yamekuwa yakikosa ajira baada ya kuhitimu nyuo mbalimbali kutokana na mifumo dume uliyopo katika sekta hizo na kuwafanya kushindwa kushiriki kikamilifu.
Mkurugenzi wa Shirika la World University
Service of Canada (WUSC) linalotekeleza mradi wa Uniterra, Manu Mwaipopo amesema hayo katika mkutano wa siku moja uliowashirikisha wadau hao jijini Arusha.
Amesema mradi huo unalenga kuyajengea uwezo  mashirika na taasisi binafsi katika kukuza fursa zilizopo katika sekta ya utalii na kilimo ili ziweze kuwasaidia vijana kupata ajira.
Mratibu wa semina ya kimataifa katika shirika hilo, Christina Sudi amesema katika programu hiyo ya kimataifa inayotekelezwa katika nchi 14 duniani, watawatumia wataalamu kutoka Canada wakishirikiana na vijana wa Tanzania kuibua fursa zilizopo katika sekta hizo.

-Mwananchi
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm